NIGERIA: MWANADADA maarufu kwenye tasnia ya muziki Barabi Afrika, Tiwa Savage amerudiana na mumewe Teebillz baada ya kuachana naye kwa kile kilichodaiwa kuwa mwanamme huyo anatumia madawa ya kulevya.
Imeelezwa kuwa, Teebillz amefanikiwa kutibiwa kisiri katika kliniki ya tiba ya madhara yatokanayo na matumizi ya madawa ya kulevya pamoja na kufanyiwa ushauri wa masuala ya ndoa (Drug Addiction Rehabilitation & Series Of Marriage Counselling).
Kwa mujibu wa televisheni moja ya nchini Nigeria humo iliyomfanyia mahojiano Tiwa, imeeleza kuwa amerudiana na mumewe huyo kimya kimya bila watu kujua kwa kile alichokieleza kuwa afya ya mumewe huyo inaendelea kuimarika baada ya kutibiwa utumiaji wa madawa ya kulevya uliokuwa umemuathiri kwa kiwango kikubwa, mbali na afya yake kuimarika, sababu nyingine ni kwamba wawili hao wanataka wamlee kwa pamoja mtoto wao wa kiume aitwae Ajmil.
Japo bado wapo kwenye harakati za mwanzo kurudiana pole pole, huku uhusiano wao ukionekana kuanza kuimarika upya siku hadi siku, wawili hao wamekuwa wakionekana kwa pamoja wakienda kwenye kituo kimoja cha ushauri wa masuala ya kisaikolojia na mambo ya ndoa jijini Lagos kwa ajili ya kupata ushauri nasaha kuhusu ndoa yao.
MZEE WA MIAKA 76 ALEYETANAGAZA KUTAFUTA MKE “FULL EXLUSIVE INTERVIEW”

