Kutoka kushoto ni Sospeter Berling, Alex Joseph, Maria Erick na Hans Frank.
Mshindi wa shindano hilo Alex Joseph (kulia) akifanya mahojiano na Global TV Online.
Mtangazaji wa Global TV Online, Kelvin Shayo akifanya mahojiano nao.
Mahojiano yakiendelea.
WANAFUNZI watano vinara wa shindano la insha kwa shule za sekondari kutoka Tanzania wameibuka kidedea baada ya kutangazwa kuwa washindi wa shindano hilo lililokuwa linajadili mada isemayo ’Jadili na taja faida na hasara za kuongeza uanachama katika umoja wa Afrika Mashariki’ ambapo iliibuka nafasi ya nne kikanda.
Wanafunzi hao ni Hans Frank (Loyola sekondari), Alex Joseph (Kibaha sekondari), Sospeter Berling (Mzumbe sekondari) na Maria Erick (Amani ya Singida).
Global TV ilikutana na wanafunzi hao waliokuwa katika Hoteli ya The Atriums, Sinza Afrika Sana jijini Dar na kufanya nao mahojiano kueleza siri ya mafanikio yao na namna walivyoweza kukabiliana na ushindani dhidi ya wanafunzi wengine kutoka nchi za jumuiya hiyo.
Washindi wa shindano hilo watazawadiwa zawadi mbalimbali kutoka kwa waandaji ikiwemo shule kunufaika na zawadi ya fedha au vifaa vya shule, wanafunzi wenyewe kupatiwa vyeti na fedha kwa mshindi wa kwanza (dola mia 300), wa pili 250, wa tatu dola 200, wa nne dola 150 na wa tano dola 100. Pia washindi hao wamemaliza ‘Tour’ ya siku tano iliyokuwa imeandaliwa na EAC Secretariat kutembelea maeneo mbalimbali kwa ajili ya kujifunza.
Mmoja wa wanafunzi hao akizungumza na mtandao huo alisema Insha hiyo ilikuwa imeandaliwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambapo mada ilitolewa Aprili hadi Juni mwaka huu kwa shule zote za sekondari hapa nchini na kutakiwa wanafunzi kuandika insha kwa kuzikutanisha shule zote za jumuiya ya Afrika mashariki.
“Nawashukuru sana walimu wangu kwa kuniwezesha kuwa miongoni mwa washindi watano kutoka hapa nchini, bila ya wao kunifundisha vizuri na kuwaelewa kwa kweli nisingeweza kuwa miongoni mwa washindi hao.
“Ushindi pia umetokana na nguvu zangu mwenyewe za kufuatilia mambo mengi yanayohusu elimu, nimekuwa nikisoma vitu vingi sana, vitabu vingi na ndio maana nimekuwa mshindi,” alisema Maria Erick.
Aidha wanafunzi hao walielezea namna walivyopokea majibu yao kwa furaha baada ya sekretarieti ya Afrika Mashariki kuwatangaza kuwa washindi, kutokana na shule zao kuwa za kawaida kabisa.
“Haikuwa rahisi kiukweli kuona nimeibuka kidedea kwani niliamini kuwa nisingeweza kuwa mshindi, nakumbuka nilivyopeleka insha yangu kwa mwalimu nilikuwa sijiamini lakini mwalimu wangu akanitia moyo yakuwa nitashinda na leo hiii kweli nimeshinda na kuipatia heshima shule yangu dah, Mungu mkubwa kwa kweli,” alisema Sospeter Berling.
Vilevile walielezea namna ilivyokuwa ngumu kwao kujua na kuelewa malengo ya Jumuiya ya nchi wanachama kutokana na uelewa wao kuwa mdogo, hususani mambo yanayohusiana na utawala wa nchi na nchi.
Makala: Denis Mtima na Kasmir Mseleche / GPL
Video: Alichokizungumza Mzee wa Miaka 76 Aliyeweka Bango Kutafuta Mwanamke wa Kuoa




