×

Gari la Kubeba Mafuta Lagonga Magari 13 na Kulipuka, Watu 33 Wafariki Dunia, 6 Wajeruhiwa

ajali kenyaajali-kenya-1ajali-kenya-2n1n2n3n5n6n7naivashapicnaivpicNAIVASHA: Watu zaidi ya 33 wameripotiwa kupoteza maisha huku wengine sita wakijeruhiwa vibaya kufuatia ajali ya gari la kubeba mafuta kutoka nchini Uganda kugonga magari mengine 13 na kulipuka moto huko Naivasha nchini Kenya jana Jumamosi, Desemba 10, 2016 usiku.

Imeelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 2:30 usiku ni gari hilo kumshinda dereva kulimudu na kuparamia magari hayo 13 kabla ya kuripuka moto pembeni mwa Barabara ya Kuu ya Nairobi-Naivasha.

Pia vyombo vya usalama barabarani nchini Kenya imesema kuwa, huenda dereva wa gari hilo lenye namba za usaliji UAK 519 C hakuwa anafahamu vizuri hali ya barabara hiyo hususani bumps (matuta) ambapo imeelezwa kuwa alikuwa akiendesha na kuruka matuta hayo kwa mwendokasi mkubwa hadi kushindwa kuumudu usukani wa gari hilo, na kusababisha ajali.

Dereva huyo amekamatwa na kufikishwa kituo cha polisi jijini Nairobi huku majeruhi wanne wakipelekwa kwenye Hospitali ya Mt Longonot Medical Centre iliyopo Naivashana kutibiwa. Wawili wametibiwa na kuruhiwa kurudi nyumbani wengine wanaendelea na matibabu. Mbali na hao wengine wawili walipelekwa hospitali ya Nairobi na wao wanaendelea na matibabu.

Aidha Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametuma salam za rambirambi kwa wafiwa na kutoa pole kwa majeruhi wa ajali hiyo ambao bado wanauguza majeraha.

CHANZO: Kenyas.co.ke

halotel-strip-1-1