×

Exclusive: Ame Ali Aitema Simba, Agoma Kurejea Kikosini

ame-ali-na-omogMshambuliaji Ame Ali amegoma kurejea katika kikosi cha Simba hivyo kuifanya klabu hiyo kuingia kwenye tafrani la kuhakikisha inasaka mshambuliaji tena.
Ame amegoma kurejea kwa madai kwamba ndani ya kikosi cha Simba hapati nafasi ya kucheza. Alijiunga na Simba kwa mkopo akitokea Azam FC lakini kuna taarifa kwamba alipewa Sh milioni 10 kwa msimu mzima.
“Kweli Ame amemueleza rafiki yake kwamba yeye harejei tena Simba. Unajua mkataba wake ni msimu mmoja tu. Hivyo kasema harudi.
 
“Viongozi wa Simba wamekuwa wakimtafuta anazungusha lakini rafiki yake baadaye katueleza kwamba harudi tena Simba kwa kuwa hapati nafasi ya kucheza,” kilieleza chanzo.
Viongozi wa Simba, wameonekana kuwa waoga kulizungumzia suala hilo, lakini mmoja wao amesema tayari juhudi za kumtaka arudishe fedha zao zimeanza.
“Kweli luna hizo taarifa, lakini kama ameamua kutorudi, poa tu. Arudishe fedha za klabu maana alilipwa kwa ajili ya msimu mzima, kacheza nusu msimu tena mechi chache. Suala la kupanga wachezaji ni la kocha, si viongozi. Hata Azam hakuwa na nafasi na aliendelea kubaki, hivyo asilete mambo ya Kiswahili hapa,” alisema.
Tokea Simba imeanza mazoezi jijini Dar es Salaam na baadaye kwenda kuweka kambi Morogoro ambako ilicheza mechi moja ya kirafiki dhidi ya Polisi Moro kabla ya kurejea Dar na kucheza na Mtibwa Sugar, Ame Ali, bado “hajaonekanaga” Msimbazi.

Darassa Afunguka Tuhuma za Kuiba Beat ya Saida Karoli Kwenye Wimbo Wake wa Muziki