×

‘Viuno Pub’ Yateketea Kwa Moto Sinza Dar

moto1-1

Gari la zimamoto likifika eneo la tukio.

moto1-2

Kikosi kazi cha zimamoto kikiwa kazini kuuthibiti moto huo.

moto1-3

Baa iliyoandikwa ‘Viuno Pub’ ikiungua eneo la Sinza-Mugabe Dar.

moto1-4

Kikosi cha zimamoto kikiendelea na kupambana na moto.

moto1-5

Mmoja wa wakazi wa eneo hilo akiwa juu ya paa la nyumba kumwaga maji.

moto1-6

Ofisa Msaididizi wa Zimamoto, Keneth Mwakasitu, akishuhudia moto huo ukizimwa.

moto1-7

Baadhi ya wananchi wakihamisha mali zao katika vibanda vyao.

moto1-8

moto1-9

Wananchi wakishuhudia tukio hilo.

moto1-10 moto1-11

Moto ukiendelea kuwaka.

Habari na Denis Mtima /GPL

BAR iliyopo eneo la kituo cha daladala cha Sinza-Mugabe jijini Dar es Salaam imeteketea kwa moto mchana wa leo kufuatia madai ya kuwepo mwanamme ambaye hakutajwa jina mara moja akidaiwa kumwaga petroli kwenye makuti ya baa hiyo na kuyawasha moto na kuondoka.

Mashuhuda wa tukio hilo waliueleza mtandao huu kuwa hakukuwa na hitilafu yoyote ya umeme katika baa hiyo bali wakadai mtu huyo alikuwa na ugomvi na mpenzi wake (wa kike) aliyekuwa akiishi maeneo ya baa hiyo na kwamba alikuwa na mwanamme mwingine.  Wamedai kwamba huenda hasira za mwanamme huyo ndizo zilisababisha kuwasha moto huo ambao umeunguza nyumba nyingi za eneo hilo.

Akizungumzia tukio hilo, Ofisa Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto aliyejitambulisha kwa jina la Keneth Mwakasitu alisema chanzo cha moto huo bado hakijajulikana kwani wahusika wa nyumba zilizoungua hawakuonekana eneo la tukio hivyo hana majibu sahihi juu ya chanzo lakini akaeleza kuwa wanaendelea na juhudi za kufahamu chanzo chake.

Kuhusiana na athari za moto huo, alisema hakuna mtu yeyote aliyeungua wala kujeruhiwa bali ni mali za wamiliki wa vibanda na vitu vya ndani ambavyo vimeungua.