×

Serikali Inawajibika Kumtafuta Ben Saanane – Lissu

lissu-global-tv-5

Tundu Lissu akiwasili kwenye Ofisi za Global Publishers.

MWANASHERIA Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu, amesema serikali ndiyo yenye wajibu wa kumtafuta na kumpata raia wake, Ben Saanane,  ambaye amepotea kwa miezi ipatayo miwili sasa.

saananeBen Saanane

Lissu ameyasema hayo wakati akizungumza na Global TV Online inayomilikiwa na kampuni ya Global Publishers, wachapishaji wa magazeti ya Uwazi, Championi, Ijumaa, Risasi, Amani na  Ijumaa Wikienda.

lissu-global-tv-8Tundu Lissu akieleza jambo.

Mwanasheria huyo alikuwa akijibu swali kuhusu ukimya wa chama chake kuhusu kada wake huyo ambaye amezua tafrani nchini akiwa hajulikani akiwa hai au amekufa.

lissu-global-tv-9Akizidi kufafanua

Alikanusha uvumi unaoenezwa kwamba huenda chama chake kinahusika katika kupotea kwa  mtu huyo, ambapo alisema katika kukwepa kusema kitu kisichojulikana, wameitaka  serikali kutoa tamko iwapo inafahamu Mtanzania huyo aliko au haifahamu.

lissu-global-tv-10“Mpaka sasa serikali haijasema lolote kuhusiana na jambo hilo.  Tunafahamu Ben amepotea lakini wakati mwingine tunanyamaza kwa sababu tunachokifahamu sisi ni sawa na mnachokifahamu nyie (waandishi wa habari) ila nawahakikishia kwamba hatuhusiki kwa vyovyote na kupotea kwake,” alisisitiza mwanasheria huyo machachari.

lissu-global-tv-12Tundu Lissu katika picha ya pamoja na Mhariri wa Gazeti la Ijumaa Wikienda, Sifael Paul.

Akisisitiza msimamo wa chama chake, alizitaka mamlaka zote husika na usalama wa raia ziseme hali halisi inayozingira sintofahamu ya mahali alipo Saanane ikiwa yuko ndani au nchi za nje, au hata kama amefariki na kuzikwa kwa kutotambuliwa.

lemaGodbless Lema alipofikishwa mahakamani. (Picha na maktaba).

Kuhusu Lema

Akizungumza kuhusu kutoonekana kwake huko Arusha kusaidia juhudi za kumpatia dhamana Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, mwanasheria huyo alisema kuna wanasheria wengi wa chama hicho wanaoweza kufanya kazi hiyo lakini akasema suala hilo linaonekana gumu kwa vile linaendeshwa kisiasa.

lissu-global-tv-13Tundu Lissu katika picha ya pamoja na Mhariri Mwandamizi wa Global Publishers, Walusanga Ndaki.

Hata hivyo, alisema ataungana na wanasheria wenzake ili kulipatia ufumbuzi suala hilo linaloonekana kuendelea bila sababu za msingi.

KESI YA FLORA MBASHA DHIDI YA MUMEWE YAFIKIA HAPA