KAGERA: Soko la Kayanga lililopo Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera limeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo huku chanzo na hasara za moto havijafahamika.
Imeelezwa kuwa ujenzi holela katika soko hilo ulikuwa kikwazo kikubwa kwa Kikosi cha Zima Moto kuweza kufika eneo la tukio na kuudhibiti moto huo.
Tukio hilo ni la pili ndani ya kipindi kisichozidi mwaka mmoja kutokea mkoani humo.