The House of Favourite Newspapers

‘Muziki’ Wazidi Kuing’arisha Nyota ya ‘Darassa’

darrrasa MKALI wa muziki wa kufokafoka (Hip Hop) nchini, Shariff Thabeet ‘Darassa’, ameendelea kuwa gumzo Afrika ya Mashariki na kila pembe ya ulimwengu kupitia mtandao wake wa YouTube. Mwanamuziki huyo mpaka sasa wimbo wake umetazamwa na watu 3,025,486, idadi ambayo imevunja rekodi kwa wanamuziki wa Bongo Fleva mwenye miondoko ya ‘Hip Hop’.drf-1darassaSoko la muziki wake limekuzwa na wimbo huo kiasi ambacho kwa sasa kila chombo cha habari kinaripoti taarifa zake. Nchi jirani kama Kenya kwa sasa wanatambua nguvu ya wanamuziki watatu hapa Tanzania, ambao ni Diamond Platnumz, Ally Kiba na Darassa.darasa2

 

Waswahili wanasema kizuri kinajiuza, kwani wimbo wa Darassa kwa sasa kila kona unasikika na kuzidi kupokelewa na watu wa kila hisia. Wimbo huo ambao haukuhitaji promo, umekuwa ukiombwa na mashabiki lukuki katika vituo mbalimbali vya televisheni  na vya redio.

Salum Milongo/GPL

Comments are closed.