






KIKOSI cha klabu ya Yanga, jana mchana kiliwasali katika Bandari ya Dar es Salaam kikitokea Visiwani Zanzibar katika michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kutolewa na watani zao Simba kwa mikwaju ya penati.
Yanga imeondolewa katika hatua ya nusu fainali kwa mikwaju ya penati 2-4 baada ya kutoka sare ndani ya dAkika 90 kwenye mchezo ambao ulipigwa usiku wa Jumanne katika Uwanja wa Amaani ambapo Simba imefanikiwa kuingia fainali na itacheza na Azam kesho Ijumaa.