×

Yaliyojiri Kwenye Mkutano wa Rais Magufuli na Wananchi wa Shinyanga

magufuli1

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kuwasalimia wananchi wa Shinyanga waliofika katika uwanja wa mpira wa Kambarage katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar mkoani humo.

????????????????????????????????????Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kuwahutubia wakazi wa Shinyanga katika kilele cha Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Kambarage mkoani humo.

magufuli4

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Shinyanga katika kilele cha maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Kambarage mkoani humo.

????????????????????????????????????

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono Kwaya ya KKKT Shinyanga mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga. PICHA NA IKULU

SHINYANGA: Katika kuadhimisha sherehe za Sikukuu ya Mapinduzi, Rais John Pombe Magufuli, leo Januri 12, 2017 ameadhimisha sherehe hizo akiwa mgeni rasmi katika Wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga na kufanikiwa kuzungumza na mamia ya wananchi wa wilaya hiyo katika waliojitokeza.

Nimekuwekea sentensi chache ikiwa ni sehemu ya hotubaya Rais Magufuli, Shinyanga leo

: Katika maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika mkoani Shinyanga, Rais ndiye mgeni rasmi.

: Naanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, nawashukuru kwa kunipa kura na nina jukumu moja tu la kuwafanyia kazi. –

: Wakati ninaomba kura nilisema nitafuata Ilani ya CCM kutekeleza yale mtakayonituma-

: Nafahamu katika siasa kila neno baya utaletewa wewe.-

: Wengine walikuwa mawaziri wa maji lakini kabla sijawa rais lakini hawakuleta maji leo wanazungumza.-

: Kupanga ni kuchagua, huwezi kununua yai kabla ya kuku anayetaga yai, litakuozea.-

: Mimi nilimchagua Makame Mbarawa kutoka Zanzibar kuja kusimamia ujenzi wa barabara huku Bara, huo ndiyo muungano.-

: Siyo lazima wote turundikane sehemu moja wakati wa sherehe hizi za Mapinduzi ya Zanzibar. –

: Suala la elimu tumeanza kutoa bilioni 11.77 kwa kila mkoa ambazo tunapeleka moja kwa moja wakuu wa shule.-

: Tumefanya hivi kukwepa minyororo ya mafisadi, fedha hizi zimesaidia kuongeza idadi ya wanafunzi mashuleni.-

: Ndege 6 tulizonunua zimetokana na makusanyo mazuri ya kodi kutoka bilioni 800 hadi trilioni 1.6 kwa mwezi. –

: Bei ya ndege kutoka Dar – Mwanza tumepunguza utoka laki 9 hadi laki 2 tu, kila mtu sasa anaweza kupanda ndege.-

: Wapo watu walizowea kula pesa za bure, ndiyo maana nikaanza nao. Nilisema atakayekosea simuhamishi kituo namtumbua hapo hapo

: Kuna watu walikuwa wanatoka Tanzania kwenda kufanya vikao nje ya nchi, nilisitisha safari zote za nje. –

: Palikuwa na wanafunzi hewa 65,000. Unatuma pesa zinaenda kuliwa na watu.-

: Tumekuta mikopo hewa ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu bil. 3.3, watu walikuwa wanakula tu. –

: Mpango wa TASAF tumekuta kuna kaya hewa 56,000. Watu walikuwa wanalipwa pesa hewa zinaenda mikononi mwa watu.-

: Eneo la Mwakitolya, aliyekuwa amepewa leseni ya kuchimba madini lazima itafutwa leseni hiyo, Watanzania wachimbe

: Nimefika Mgodi wa Maganzo, kuna matatizo ya ardhi, nimeagiza yashughulikiwe haraka.-

: Wanaosema nakosea kutumbua majipu basi wao ndiyo majipu, walikuwa wanapiga pesa za serikali.-

: Naagiza Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Viwanda kufutwa kwa mradi wa mwekezaji wa Triple S wa kiwanda cha Nyama, Shinyanga.

: Hatuwei kusubili mwekezaji kwa zaidi ya miaka 10 bila mafanikio, tunataka Tanzania mpya yenye maendeleo.-

: Nimeambiwa kuna tatizo la bei ya maji hapa Shinyanga.-

Tatizo la bei ya maji

: Endapo nitakuta bei ya maji Shinyanga ni kubwa kuliko maeneo mengine nitashusha, kama ni ndogo nitapandisha.-

Rais Magufuli akamsimamisha Mbunge wa Shinyanga ili amueleze bei ya maji inayolalamikiwa na wananchi.

Mbunge wa Shinyanga amemeleza Rais Magufuli kuwa bei ya maji kwa Mkoa wa Shinyanga ni kubwa kuliko maeneo mengine ya nchi kwa sababu gharama zote za kuendesha mtambo wa mradi wa maji unaosambaza Kahama na Shinyanga (KASHWASA) zimebebeshwa kwa wananchi.

Mhandisi wa Maji wa Mkoa wa Shinyanga anajibu

Bei kwa Uniti 1 ya maji kwa mikoa mingine ni kama ifuatavyo.

Dar es Salaam ni Tsh. 1668

Bukoba Tsh 1225

Iringa Tsh 1345

Tanga Tsh 1160

Singida Tsh 1120

Shinyanga Tsh 1000

Hivyo Shinyanga tuna bei ndogo kuliko mikoa baadhi mingine.

Baada ya hapo Rais Magufuli akatoa auli yake.

: Nimewasikiliza mbunge na mhandisi, naomba wananchi niachieni na mimi nikacheki nitalishughulikia swla hili.-

: Vikundi vitano vilivyokuwa wakitumbuiza hapa jukwaani nitawapa milioni 1 mtagawana.-

: Anawashukuru wananchi na kuwaaga, Mkutano wa Rais na wananchi Shinyanga umefungwa rasmi.