The House of Favourite Newspapers

MJ Records Yatambulisha Kundi Jipya la Bongo Fleva

mj-records-1

Lebo maarufu ya muziki hapa Bongo, MJ Records imetambulisha kundi lake jipya la muziki wa Bongo Fleva ambalo ni Hanike Band. Kundi hilo linayotokana na muungano wa wasanii watatu ambao ni Haithamkim, Nini Tz pamoja na Kella Tz.

Akizungumza na Mtandao wa Global Publishers, producer wa MJ Records, Daxo Chali ambaye pia ni mdogo wa Marco Chali, ameeleza ujio wa band hiyo mpya kwenye game ya Bongo Fleva.

mj-records-3Kutoka kushoto ni Nini_Tz, Kellah_Tz na Haitham Kim

“Hanikeband ni kundi zao jipya ambalo limeunda ndani ya MJ Records, na limetokana na kuungana kwa  Haithamkim , Nini Tz na Kellah Tz, tunatarajia kuona mambo mazuri kutoka kwenye combination hii kuanzia mwaka huu wa 2017.”

mj-records-2

Wakiwa na producer, Daxo Chali.

Alichokiandika nini Instagram:

‘2017 🔥🔥Kutoka @mjrecordstz @haithamkim , @nini_tz Na @kellah_tz Wameungana Nakuunda Kundi Linaloitwa @hanikeband SUPPORT #VIPAJIMAALUMU Cc; @marcochali @masterjtz

Comments are closed.