
Khadija Naif alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar akitokea Dubai.
DAR ES SALAAM: Mtanzania wa kwanza ambaye amepewa heshima ya kuwa balozi wa WGFA, na Mwafrika wa pili kupata heshima hiyo, Khadija Naif, amerejea nchini jana akitokea nchini Dubai, alipopata ubalozi huo kutokana na kujitoa kwa moyo kwa wajasiriamali wadogowadogo.

Khadija Kushoto Akipokea zawadi kutoka kwa mmoja wa wadau waliofika kumpokea.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar, Khadija alisema kuwa ubalozi alioupata ni kwa ajili ya Watanzania wote kwa kuwa ameleta heshima nyumbani na anajivunia kuwa Mtanzania wa kwanza kupata heshima ya ubalozi huo.

Akiwa katika picha ya pozi baada ya kuwasili.

Khadija Naif Akionesha Cheti cha Ubalozi.

Mmoja wa wajasiliamali waliokuja kumpokea akionesha cheti hicho pia.

Khadija Naif watatu kutoka kushoto na wadau katika picha ya pamoja.
“ Ninafurahi sana ni kitu kizuri na ni moja ya kuipa heshima nchini yangu na nitaendelea kujitolea,” alisema.
Imelda Mtema/GPL