SENEGAL: RAIS Mteule wa Gambia, Adama Barrow amesema kuwa ataapishwa leo jioni kuwa rais wa nchi hiyo, kwenye Ubalozi wa Gambia ulio kwenye nchi jirani ya Senegal kama ilivyopangwa.
Ujumbe ulioandikwa kwenye akaunti za Adama Barrow za mitandao ya kijamii uliiwaalika watu kuhudhuria sherehe hiyo.
Kufuatia kushindwa katika uchaguzi mwezi uliopita na kukataa matokeo ya uchaguzi huo, Rais Yahya Jammeh amegoma kuondoka madarakani huku jitihada za mwisho za viongozi wa kanda za kumshawishi zikikwama.
Vikosi vya wanajeshi wa nchi za Afrika Magharibi viko tayari kushinikiza mabadiliko ya mamlaka nchini Gambia, nchi ambayo ni maarufu kwa watalii. Wakai huo, vikosi vya Senegal vimesalia kwenye mpaka na Gambia huku muda wa mwisho wa Jammeh kuondoka madarakani ukikamilika usiku wa manane. Hatua za kijeshi zinaungwa mkono na Nigeria pamjaa na nchi zingine ukanda huo.
Barrow amekuwa nchini Senegal tangu Jumapili baada ya mwaliko kutoka kwa viongozi wa nchi za Afrika, wanaounga mkono ushidi wake.
Barrow aliandika katika mtandao wa Twitter na Facebook akisema kuwa ataapishwa majira ya saa 16:00 GMT (1:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki) kwenye Ubalozi wa Gambia mjini Dakar, Senegal.
Takriban watu 26,000 nchini Gambia, walio na hofu kuwa kutazuka ghasia, wamekimbilia usalama nchini Senegal. Watalii kutoka Uingezrea na Uholanzi wanazidi kuondolewa kutoka taifa hilo la Magharibi mwa Afrika.