The House of Favourite Newspapers

Ditto Kumtoa Afande Selle 2017

ditto-1

Lameck Ditto (kushoto) akiongea na Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally (kulia).

Mkali wa Bongo Fleva anayetikisa kwa sasa na wimbo wake ‘Moyo Sukuma Damu’, Lameck Ditto, amesema yupo katika mchakato wa kurudisha utaratibu wa albamu na katika albamu yake mpya upo wimbo alioshirikiana na Mfalme wa Mashairi, Selleman Msindi ‘Afende Selle’.

ditto-6

Ujio wa albamu hiyo utamrudisha Afande Selle kwenye game na Ditto anaamini msanii huyo ana uwezo mkubwa sana na mwenye heshima katika sanaa. Kibao hicho kitamrudisha Afande Sele na ataweza kuwa bora kama zamani.

ditto-10

Aidha Ditto ameendelea kutajwa kama mwandishi bora kutoka Jumba la Vipaji Tanzania (THT) ambapo ameandika nyimbo nyingi kama vile ‘Malkia Wa Nguvu’ wa Estelina Sanga ‘Linnah’ na nyingine nyingi.

Salum Milongo/GPL

 

 

 

Comments are closed.