
USHAHIDI dhidi ya aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mataka, umeendelea leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kamera yetu kumnasa akitoka kujibu kesi yake ya tuhuma za kughushi na matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara 

Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mataka, akishuka ngazi za Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo wakati wa kusikilizwa kwa kesi yake iliyoahirishwa.
Kesi hiyo imeahirishwa leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Respicius Mwijage, hadi Machi 3 mwaka huu kwa ajili ya kuendelea na ushahidi wa serikali dhidi yake.
Na Denis Mtima/GPL