
Rais Mteule wa Marekani Donald Trump.
RAIS WA MAREKANI Donald Trump amefanya kile alichokiita siku yake ya kwanza kuanza kazi katika utawala wake, kutokana na maamuzi aliyoyafanya ya nchi yake kujiondoa katika mpango wa Ushirikiano wa kiuchumi wa nchi zinazounganishwa na bahari ya Pasifiki. 
Rais Mteule wa Marekani Donald Trump.
Ameonya pia kuyapa adhabu makampuni ya nchi hiyo yanayopeleka kazi nje ya nchi.
Makubaliano ya Mpango wa Ushirikianio wa Kibiashara wa nchi zinazounganishwa na Bahari ya Pacific TPP, yalijadiliwa na utawala wa Rais Barack Obama.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani Sean Spicer anasema hatua hiyo ni dalili ya kuanza kwa enzi mpya ya sera za biashara za Marekani.
”…Kama alivyokuwa akisema Rais mara nyingi, hii ni aina ya makubaliano ya mataifa mengi na si kwa maslahi mazuri kwetu, na amekua akienda haraka kuboresha sera za kibiashara ambazo zitaongeza ushindani wa wafanyakazi wa Marekani na uzalishaji…” Alisema Sean Spicer
Amesema amri hiyo ya Rais inaongoza katika enzi mpya ya sera za biashara ya Marekani, ambayo utawala wa Trump utapata fursa ya kufanya biashara na washirika wake duniani kote.