Maimartha Atoa Fundisho Kwa Wanaojitapa Kuhusu Wapenzi Wao
Global Publishers January 25, 2017
SHARE THIS:
Maimartha Jesse.
MTANGAZAJI na Mshereheshaji wa vipindi vya Televisheni Bongo Maimartha Jesse jana ameandika ujumbe mwenye fundisho kwa watu walio katika mahusiano, ujumbe huo ni huu…
“Mke wa Kelvin anajivunia mume mtulivu, hashindi baa na hatongozi videmu. Akitoka kazini huenda kucheza basketball na hurudi nyakati za dinner. Siku moja mkewe akamhurumia. Anachoka na kazi. Mtu gani asiyependa starehe japo kidogo? Mke akamlazimisha outing, Kelvin akabisha lakini taxi ikafika.
Gonga Club & Lodge. Walipofika mlangoni tu, mlinzi akaita, Mambo Kelvin! Poa Nilidhani huwa huji club, inakuwaje mlinzi anakufahamu? mke akauliza Yule mgambo, mchana analinda ofisini kwetu, usiku anapiga part time hapa akajibu Kelvin.
Maimartha Jesse.
Wakachagua meza. Kukaa tu tayari mhudumu ameshaleta castle lager. Akamuuliza mama anakunywa nini. Mhudumu alipoondoka mama akauliza, amejuaje unakunywa castle kama hakufahamu? Wakati Kelvin anajikanyaga aanze vipi kujitetea, mhudumu wa vyumba akawa amefika na kuuliza.