×

Mambo Yaanza Kunoga Shinda Nyumba Watu Kulamba Pikipiki, Tv, Simu

shinda-nyumba-1

Wasomaji wa magazeti ya Global wakiwa katika pozi baada ya kujaza kuponi ya Shinda Nyumba awamu ya pili.

shinda-nyumba-5

shinda-nyumba-13

Mr Uwazi akiendelea kugawa zawadi mbalimbali za Shinda Nyumba.

shinda-nyumba-7

shinda-nyumba-14

Wasomaji wakivaa T-shirt za Shinda Nyumba baada ya kukabidhiwa.

shinda-nyumba-9 shinda-nyumba-10 shinda-nyumba-11 shinda-nyumba-12

shinda-nyumba-28 Kupon zikiendelea kujazwa. shinda-nyumba-18 shinda-nyumba-19 shinda-nyumba-20

Zawadi zikiendelea kutolewa kwa wasomaji.

shinda-nyumba-23 shinda-nyumba-27

Wananchi wakiendelea kupewa elimu ya kushiriki Shinda Nyumba awamu ya pili.

ILE Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba awamu ya pili imeanza kunoga kwani droo ya kwanza ya kihistoria inatarajiwa kufanyika Februari 8, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdalah Mrisho alisema jana kuwa droo hiyo ya kwanza ndogo, itawapata washindi wanne ambao watajishindia pikipiki, televisheni, simu za kisasa (Smartphones) na vyombo vya ndani.

“Wasomaji wahakikishe wanajipatia kuponi za kutosha tayari kwa droo yetu ndogo ya kwanza ambayo itafanyika hiyo Februari 8, mwaka huu. Kama wanavyoona, katika siku yake ya kwanza tu, tunatoa zawadi hizi ambazo zinatosha kabisa kubadilisha maisha ya mshiriki, huu si wakati wa kuupoteza.

“Sehemu hasa itakapofanyika droo hii tutaitangaza ndani ya muda mfupi ujao, lakini kwa vyovyote itakuwa ni hapa Dar es Salaam, utaratibu wetu wa kutuma kuponi ni uleule, baada ya kununua gazeti letu lolote kati ya Championi, Risasi, Uwazi, Amani, Ijumaa na Ijumaa Wikienda, kata kuponi kisha jaza kwa kadiri ilivyoelekezwa, halafu peleka kwa wakala yeyote aliye jirani na wewe, maana mawakala wetu wapo nchi nzima, au kwa wale wa Dar es Salaam, wanaweza kuzileta katika ofisi zetu zilizopo Bamaga, Mwenge,” alisema.

Wakati hayo yakitangazwa, miji ya Mbeya, Arusha na Mwanza, kwa nyakati tofauti wiki iliyopita, nayo ilifanya uzinduzi wa promosheni ya shindano hilo, huku wasomaji wakazi wa maeneo hayo, wakisisitiza kuwa hii ni zamu yao ya kuibuka washindi baada ya Nelly Mwangosi wa Iringa kupata nyumba ya mamilioni mwaka jana.

“Kabla ya kupatikana kwa mshindi, tulijua haya ni mambo ya mipango tu, si unajua tena maana haikuwahi kutokea kampuni ya magazeti ikatoa zawadi kubwa kiasi kile, kwa hiyo wengine tukaona hebu acha tuone, lakini baada ya mshindi kupatikana, tumegundua hii kitu ilikuwa ni kweli,” alisema Joshua Laiser wa Kijenge mkoani Arusha.

Laiser alisema mwaka huu utakuwa ni msimu wa watu wa Kanda ya Kaskazini na bila shaka, yeye ndiye atakuwa mshindi kwa niaba yao.

“Nimekuwa mteja wa muda mrefu wa magazeti ya Global Publishers ila nilikuwa sitilii maanani mashindano yaliyokuwa yakiendeshwa kutokana na kutoamini kama mshindi anapatikana bila kupangwa, ila baada ya kuona mshindi wa awamu ya kwanza kapatikana kutoka Iringa, tena ni mwanamke mjasiriamali, nikashawishika sana na sasa tutakula sahani moja mpaka kieleweke,” alisema Laiser.

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam