WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), George Simbachawene, leo amekazia tena agizo alilolitoa jana la kutaka Wamachinga kuondoka kwenye maeneo ya miundombinu ya mabasi yaendayo haraka (BRT) ‘mwendo kasi’ kwa kuwapa siku tatu la sivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Simbachawene alisisitiza hayo jijini Dar es Salaama akirejea hotuba aliyoitoa jana kwenye uzinduzi rasmi wa mabasi yaendayo haraka uliofanyika jana katika kituo cha mabasi hayo cha Gerezani-Kariakoo, jijini Dar, ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais John Magufuli alikuwa mgeni rasmi.
“Niwaagize wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kulisimamia hili kuhakikisha wafanyabiashara (Wamachinga) wanaondoka katika kingo za barabara za mabasi ya mwendo wa haraka kuanzia Kimara, Manzese, Kariakoo, Feri na kwingineko.
“Kumekuwa na ajali zisizo za lazima kwa watu mbalimbali wanaoingilia miundombinu ya mabasi hayo kugongwa na vioo vya mabasi (side mirrors) jambo ambalo ni hatari sana.
“Kwa mtu ambaye atakiuka agizo hilo basi akamatwe na wenye magari yao yatolewe matairi au upepo kama ambavyo Rais Dk. Magufuli alisema jana,” alisisitiza Simbachawene.
NA DENIS MTIMA/GPL