Mwandishi Wetu
TIMU ya soka ya Global Publishers, leo Ijumaa inatarajiwa kujitupa uwanjani kuonyeshana umwamba na Sinza Veteran.
Global itavaana na Sinza Veteran katika mcheo wa kirafiki kwenye Uwanja wa CCM Sinza Lion jijini Dar. Nahodha wa Global, Phillip Nkini amesema maandalizi kwa upande wao yapo vizuri wakiwa chini ya kocha Saleh Ally na lengo lao ni kuibuka na ushindi.
“Tumejiandaa vizuri na maandalizi tuliyoyafanya yanatupa uhakika mkubwa wa kushinda pambano letu hili la leo na kikosi kizima kipo vizuri,” alisema.