×

Vyakula vinavyosaidia kuzuia, kukinga vidonda vya tumbo

MAFUTA NA NAZIVYAKULA vifuatavyo husaidia kutibu au kukinga ugonjwa wa vidonda vya tumbo (perptic alcers) kama vitatumika ipasavyo. Kitunguu Saumu Kitunguu saumu husaidia kutibu vidonda vya  tumbo. Watafiti katika kituo cha utafiti wa kansa cha Fred Hutchinson Cancer Research Center, Seattle Washington, Marekani waligundua kuwa uwezo ambao kitunguu saumu unacho katika kudhibiti na kuua bakteria mbalimbali mwilini unaweza kudhiti pia bakteria anayesababisha vidonda vya tumbo mwilini ajulikanaye kama Helicobacter Pylori (H. pylori).

Chukuwa punje sita hadi 10 za kitunguu saumu, menya na ukate vipande vidogo vidogo kisha umeze pamoja na maji vikombe viwili kutwa mara mbili kwa wiki mbili au tatu. ASALI Asali mbichi ina uwezo mkubwa katika kutibu vidonda vya tumbo.

Asali ni dawa karibu kwa kila ugonjwa. Kuna kimeng’enya kilichomo kwenye asali kijulikanacho kama ‘glucose oxidase’ ambacho huizalisha ‘hydrogen peroxide’ ambayo yenyewe inayo uwezo wa kuuwa bakteria wabaya mwilini ambao husababisha vidonda vya tumbo.

Pia hii ‘glucose oxidase’ huulainisha ukuta wa tumbo na kupunguza muwako au vidonda tumboni. Lamba vijiko vikubwa viwili kutwa mara tatu au vijiko vikubwa vitatu kutwa mara mbili. Itasaidia kusafisha tumbo, itaimarisha ukuta wa tumbo na kuzuia na kutibu vidonda vya tumbo. Fanya hivi kwa wiki tatu hadi nne. Hakikisha unapata asali mbichi salama ambayo haijachakachuliwa.

KABEJI Kabeji inaweza kutibu vodonda vya tumbo kwani inayo ‘lactic acid’ na husaidia kutengeneza amino asidi ambayo huhamasisha utiririkaji wa damu kwenda kwenye kuta za tumbo jambo linalosaidia kuuongezea nguvu ukuta wa tumbo na hatimaye kutibu vidonda vya tumbo.

Kabeji pia ina kiasi kingi cha vitamini C ambayo imethibitika kuwa na faida kubwa kwa watu wenye vidonda vya tumbo vilivyosababishwa na maambukizi ya bakteria aitwaye H. pylori. Kata kabeji nzima mara mbili na uchukue nusu yake, chukuwa karoti mbili na ukatekate vipande vidogo vidogo na utumbukize vyote, kabeji na karoti  kwenye ‘blenda’ na uvisage (au saga kwa njia yoyote) ili kupata juisi yake.

Kunywa kikombe kimoja cha juisi hii kila nusu saa kabla ya chakula cha asubuhi, mchana na jioni na kikombe kimoja kabla hujaenda kulala. Imethibitika kuwa juisi ya karoti freshi inayo vitamini U muhimu kwa ajili ya kudhibiti vidonda vya tumbo. Rudia zoezi hili kila siku kwa wiki kadhaa na hakikisha unatumia juisi freshi utaona faida yake.

NDIZI

Ndizi zilizoiva na hata ambazo hazijaiva zote ni nzuri kwa ajili ya kudhibiti vidonda vya tumbo. Kuna aina maalumu ya muunganiko wa vimeng’enya vilivyomo kwenye ndizi ambavyo huzuia kuongezeka au kuzaliana kwa bakteria wa vidonda vya tumbo waitwao H. Pylori.

Ndizi pia huulinda mfumo wa kuta za tumbo kwa kuiondoa asidi iliyozidi tumboni na hivyo kusaidia kuuondoa uvimbe au vidonda tumboni na pia kuuongezea nguvu ukuta wa tumbo. Ili kutibu vidonda vya tumbo, kula angalau ndizi zilizoiva tatu kwa siku au menya ndizi mbili au tatu na uzikate katika vipande vidogo vyembamba (slices) na uanike juani mpaka zikauke kabisa.

Kisha saga vipande hivyo ili kupata unga na uchanganye vijiko vikubwa viwili vya unga huu na kijiko kikubwa kimoja cha asali na ulambe mchanganyiko huu mara tatu kwa siku kwa wiki mbili.

UNGA MAJANI YA  MLONGE Mlonge ni mti muhimu sana katika utabibu kama tiba mbadala, majani, maua, mbegu na mizizi yake hutumika sana katika kutibu  magonjwa mbalimbali. Mlonge una kiasi kingi cha vitamin C, Madini ya chuma, protini, Vitamini A na potasiamu.

Ongeza kijiko kimoja cha chakula kwenye bakuli ya mboga unapokula chakula cha mchana na jioni. Unaweza pia kunywa unga huu wa mlonge pamoja na juisi yoyote uliyotengeneza mwenyewe nyumbani au unaweza kuuchanganya kwenye chakula kama vile wali na hivyo ukajiongezea kinga zako dhidi ya vidonda vya tumbo. Tumia kwa wiki tatu hadi  nne.

NAZI

Nazi ni nzuri sana katika kutibu vidonda vya tumbo sababu ya sifa yake na uwezo wa kuua bakteria. Nazi huziua bakteria zinazosababisha vidonda vya tumbo. Pia tui la nazi na maji ya nazi (dafu) vyote vina sifa na uwezo wa kutibu vidonda vya tumbo. Kunywa vikombe kadhaa vya tui freshi la nazi au maji ya nazi kila siku. Pia unaweza kuitafuana nazi yenyewe mara kwa mara. Fuatisha mlolongo huu walau kwa wiki mbili ili kupata matokeo chanya. Au kunywa kijiko kikubwa kimoja cha mafuta ya asili ya nazi asubuhi kabisa na kingine usiku kwa wiki mbili.

UWATU

Uwatu unajulikana sana kwa uwezo wake wa kutibu maradhi mengi mwilini. Unaweza pia kuutumia katika kutibu vidonda vya tumbo. Kwa kuwa uwatu inayo gundi maalumu au ulimbo ambayo huulinda ukuta wa tumbo kwa kuufunga au kuufunika kama utando hivyo kurahisisha hatua za kutibu vidonda vya tumbo.

Chemsha mbegu za uwatu kijiko kidogo cha chai ndani ya vikombe viwili vya maji, chuja na uongeze asali kidogo na unywe kwa pamoja kutwa mara mbili kwa wiki mbili. Unaweza pia kutumia kijiko kidogo kimoja cha chai cha unga wa mbegu za uwatu ukichanganya kwenye kikombe cha maziwa ya moto.

Au unaweza kuchemsha kikombe kimoja cha majani freshi ya uwatu, ongeza asali kidogo na unywe mara 2mbili kwa siku kwa wiki mbili au tatu. Ingawa maziwa hayashauriwi sana kutumika kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo, hivyo unaweza kutumia maji ya uvuguvugu badala ya maziwa kama vidonda vyako vimeshakuwa sugu sana au ikiwa unahitaji upate nafuu ya haraka na hatimaye kupona. Usisahahu pia kunywa maji ya kutosha kila siku.