×

Azam uso kwa uso na mabingwa wa Afrika leo usiku

Azam FC

Na Mwandishi Wetu

TIMU ya Azam FC, leo saa 1:00 usiku, inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Mabingwa wa Afrika, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Mamelod Sundowns

Hii ni mara ya pili kwa timu hizo kukutana kwenye mechi ya kirafiki ambapo Agosti 7, 2013 zilikutana kwa mara ya kwanza nchini Afrika Kusini wakati Azam FC ilipoenda kuweka kambi ya maandalizi ya msimu mpya na kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Mamelodi ambayo imekuja hapa nchini juzi Jumatatu kuweka kambi, inajiandaa na mchezo wa Super Cup dhidi ya mabingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika, TP Mazembe ya DR Congo, utakaopigwa Februari 18, mwaka huu. Mbali na kucheza na Azam, pia inatarajiwa kuvaana na African Lyon, mchezo utakaopigwa Alhamisi ya Februari 9, mwaka huu.