
Afisa Masoko wa Global Publishers, Jimmy Haroub (kushoto) akimsaidia msomaji Jonathan Mchuruza wa Sokota, Temeke kujaza kuponi.

Mr Shinda Nyumba akiwa na msomaji, Mama Hadija wa Sokota




Wasomaji mama Hadija akiwa na mwenzake, mama Nahd wa Sokota, Temeke


WAfanyabiashara wa mbao wa Keko wakiwa na Jimmy



Mr Shinda Nyumba ameibukia maeneo ya Keko Magurumbasi, Machungwa, Sokota Temeke, Mtaa wa Yombo jijini Dar na kwingineko ambapo amewahimiza wasomaji kuendelea kujaza kuponi pamoja na kukusanya zingine kwa ajili ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba.
Wasomaji wa maeneo hayo wamefurahishwa kumuona mubashara Mr Shinda Nyumba huku wengine wakinunua kwa wingi magazeti pamoja na kujaza kuponi zao.
Akizungumza na mtandao huu, mmoja wa wasomaji wazuri wa Magazeti Pendwa, Rehema Hassan alisema kuwa amejipanga vizuri katika kuhakikisha anashinda nyumba ya mwaka huu.
“Nimedhamiria kuhakikisha namiliki nyumba ya mwaka huu na kila siku sikosi kununua Magazeti Pendwa na kujaza kuponi,” alisema Rehema Mkazi wa Temeke, Dar.
Habari/picha na Gabriel Ng’osha/GPL