The House of Favourite Newspapers

New: Sarkodie Anaisogeza Kwetu ‘S.H.O.U.T’ Rap Version Ya ‘Overnight Celebrity’ – (Audio)

 

Siku zote kitu kizuri share na mwenzako. Nimekutana na mdundo mpya ‘S.H.O.U.T’ wa rapa Sarkodie kutoka Ghana na jinsi alivyotembea na beat nikaona why not nisishare na wewe…

Mmiliki wa lebo ya Sarkcess Music, Sarkodie ameachia rap version yake ya dakika tatu ya wimbo wa Twista ‘Overnight Celebrity’ na kuupa wimbo huo jina la ‘S.H.O.U.T’. Unaweza usimuelewe anaimba nini lakini ukiisikiliza ngoma hii mwanzo mwisho na kwa umakini utapenda jinsi ambavyo rapa huyo ametembea na instrumentals za wimbo huo maana bars anazoziachia humo ndani ni za kuotea mbali.

‘Overnight Celebrity’ ni wimbo ulioimbwa na msanii kutoka Marekani Twista na unapatikana kwenye album yake ya 2004 iitwayo ‘Kamikaze’. Wimbo huo ulifanikiwa kugusa Top 10 ya Billboard Hot 100 May 11 2004 na kukaa kwenye nafasi ya sita kwa wiki kadhaa.

SARKODIE – S.H.O.U.T.

 

IMEANDIKWA NA: Sandra Brown.

Comments are closed.