×

Wasanii Wawili Kumenyana Fainali ya Wikienda Music Search (WMS)

Baadhi ya washiriki wa Shindano la Wikienda Music Search wakiwa kwenye pozi na Produzya Shentee Murozi, (mwenye fulana ya zambarau).

WASANII wawili wa Muziki wa Bongo Fleva, wamefanikiwa kuingia kwenye fainali ya Shindano la Wikienda Music Search (WMS) linaloendeshwa na Gazeti la Ijumaa Wikienda baada ya kupita kwenye mchujo uliofanyika leo kwenye Studio za Black zilizopo Magomeni- Kagera jijini Dar.

Mwanadada Leila Joackimu akionyesha uwezo wake.

Wasanii hao ni Alen Venance kutoka Ilala na Frank Mgogosi wa Kimara ambao wamewamwaga wasanii wenzao 18 akiwemo mwanadada mmoja.

Mkali wa kurap Akida kutoka Kigamboni akifanya yake.
Mmoja wa wasanii Frank Mgogosi wa Kimara, Dara amefanikiwa kuingia fainali.
Msani Alen Venance kutoka Ilala, Dar naye amefanikwa kuingia fainali.
Baadhi ya wasanii wengine wakifanya yao mbele ya majaji hawapo pichani.
Baadhi ya wasanii wengine wakifanya yao mbele ya majaji hawapo pichani.
Baadhi ya wasanii wengine wakifanya yao mbele ya majaji hawapo pichani.
Msanii Peter Mwaisomania kutoka Mbeya akiimba.

Washindi hao wawili watapambana hivi karibuni kwenye Studio za Wanene Entertainment zilizopo Mwenge jijini Dar.

Mratibu wa WMS, Gabriel Ng’osha, amewashauri wasanii wa kike kujitokeza kwa wingi zinapotokea fursa za sanaa, ujasirimali na nyinginezo, ili kuweza kufikia ndoto zao kwani hakuna anayefahamu atafanikiwa kwa njia gani.

Shindano hili limeandaliwa na Gazeti la Ijumaa Wikienda na kudhaminiwa na Studio ya Black na Wanene Entertainment.

Habari/Picha:Gabriel Ng’osha/GPL