The House of Favourite Newspapers

Uvimbe kwenye kizazi cha Mwanamke Janga kuu kwa sasa

KUNA AINA KUU ZIFUATAZO ZA FIBROIDS:

1. Submucosal Fibroids ndani ya kizazi.

2. Intramural Fibroid ndani ya nyama za kizazi.

3. Subserosal nje ya kizazi.

Watu wafuatao wako hatarini kupata ugonjwa huu wa Fibroids.

1. Mwanamke ambaye hajawahi kupata mtoto mpaka umri mkubwa.

2. Kuanzia kubalehe mpaka hedhi kukoma.

3. Kurithi

4, unene

5, kuingia hedhi mapema.

Fibroids siyo kansa ni uvimbe wa kawaida tu ambao unakua kwa kutegemea kichocheo cha Estrogen Hormone ndiyo maana kuanzia kubalehe mpaka kukoma kwa hedhi ndiyo wako hatarini.

Na mara nyingi uvimbe huwa  unaongezeka kukua sana hasa wakati wa ujauzito kwani vichocheo hivi huongezeka wakati huu kulinda makazi ya mtoto. Wanawake waliofikia kikomo cha hedhi huwa hawapati Fibroids au kitaalam Leomyoma .

DALILI ZA FIBROIDS

1. Kutokwa damu kwenye via vya uzazi katikati ya mwezi.

2. Kutokwa na uchafu wenye harufu mbaya au ambao hauna harufu lakini mwingi na mweupe.

3. Maumivi ya kiuno hasa wakati wa hedhi ambayo husababishwa na kizazi kujaribu kusukuma huo uvimbe, wengi hupata maumivu makali sana.

4. Tumbo kuuma sana chini ya kitovu.

5. Hedhi zisizokuwa na mpango.

6. Maumivu wakati wa tendo la ndoa.

7. Kukosa hamu ya tendo la ndoa.

8. Maumivu makali wakati wa hedhi.

Uvimbe unapokua mkubwa unaweza kusababisha dalili zifuatazo;

1. Kukojoa mara kwa mara kwani uvimbe unakandamiza kibofu cha mkojo

2. Mkojo kubaki kwenye kibofu cha mkojo.

3. Haja kuwa ngumu.

4. Miguu kuvimba.

5. Kupungukiwa damu.

JINSI FIBROIDS ZINAVYOWEZA KUZUIA KUPATA MTOTO:

1. Fibriods zikikua sana zinakandamiza mishipa ya kupitisha mayai kutoka kwenye kiwanda yaani ovari.

2. Uvimbe pia unazuia yai lililorutubishwa kujishikiza kwenye kizazi hasa Submucosal Fibroids.

3. Pia huzuia mfuko wa kizazi kukaza kusukuma mbegu kwenda kwenye mishipa ya kupitisha mayai.

MATIBABU

1. Wanawake wengi wana Fibroids ndogondogo lakini kwa sababu hazina dalili hawawezi kwenda hospitali na hawa ndiyo siku wakibeba ujauzito uvimbe unaongezeka kwa sababu ya vichocheo kuongezeka hivyo hawa watu tunawabaini tunapofanya ultrasoudi

Comments are closed.