
Na Mohammed Masoud, DODOMA
KATIKA vita inayoendelea nchi nzima dhidi ya matumizi ya vifungashio vya pombe aina ya Viroba zilizopigwa marufuku na serikali, Jeshi la Polisi mkoa wa DODOMA limekamata shehena ya pombe kali za viroba kwenye gala la Kampuni ya Mselia Enterprises huku likidhibitisha kuwa mmiliki wa ghala hilo kujiua kwa kujipiga risasi baada ya shehena yake hiyo kukamatwa.
Mfanyabaishara huyo aitwae FESTO MSELIA aliyejiua ni wakala mkuu wa usambazaji wa pombe hizo ambapo alikuwa akimiliki shehena ya pombe hizo zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1, kukiwa na zaidi ya katoni 1400 za viroba katika moja ya stoo zake.
Awali katika operesheni hiyo iliongozwa na kamanda wa polisi mkoa wa DODOMA LAZARO MAMBOSASA Mambosasa ambapo alimtaka aendelee na shughuli zake na akaamuru shehena hiyo isiuzwe wala kutumika akisubiri maelekezo.
Jeshi la Polisi mkoa wa DODOMA limedai kuwa taarifa rasmi juu ya tukio la mfanyabiashara huyo itatolewa mara baada ya uchunguzi rasmi kukamilika.
NIMEKUWEKEA HAPA VIDEO YAKE