×

PSG Kamwe Hawatakisahau Kipigo cha Barcelona UEFA

  

KLABU ya Barcelona wametinga nusu fainali kwa kuigonga Klabu ya Paris Saint Germain (PSG) kwa mabao 6-1 katika mchezo wa marudiano wa Klabu Bingwa Ulaya usiku wa kuamkia leo, kichapo ambacho kamwe PSG hawatokisahau.

Sergi Roberto alifunga bao la 6 kwa mkwaju wa mwisho wa mchezo, na hivyo kufanya matokeo ya jumla kuwa 6-5 kwenye mchezo uliopigwa kwenye dimba la Nou Camp.

Barcelona walifunga magoli matatu katika dakika saba za mwisho. Walikuwa wakiongoza kwa 3-1. Wiki tatu zilizopita PSG iliifunga Barcelona magoli 4-0 mjini Paris.

Hatua ya kurejesha magoli yote hayo ni kubwa kuwahi kushuhudiwa katika historia ya UEFA, na sasa Barcelona wana kila nafasi ya kunyanyua kombe la Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka mitatu.

Katika mchezo mwingine, Pierre Emerick Aubameyang alipachika ‘hat trick’ na kuipeleka Borussia Dortmund katika robo fainali dhidi ya Benfica. Borussia Dortmund wameshinda kwa jumla ya magoli 4-1 katika mechi mbili walizocheza.

Barcelona: ter Stegen, Rafinha (Sergi Roberto 76), Umtiti, Pique, Mascherano, Iniesta (Turan 65), Busquets, Rakitic (Andre Gomes 84), Neymar, Luis Suarez, Messi

Subs not used: Cillessen, Alcacer, Jordi Alba, Digne

Goalscorers: Suarez 3, Kurzawa og 40, Messi 50, Neymar 88, 90, Sergi Roberto 90+5

Booked: Pique, Busquets, Rakitic, Suarez, Neymar

PSG: Trapp, Meunier (Krychowiak 90), Marquinhos, Thiago Silva, Kurzawa, Lucas Moura (Di Maria 55), Rabiot, Matuidi, Draxler, Verratti, Cavani

Subs not used: Areola, Kimpembe, Krychowiak, Pastore, Aurier, Ben Arfa

Goalscorers: Cavani 62

Booked: Matuidi, Draxler, Cavani, Marquinhos, Verratti

Referee: Deniz Aytekin