

Global Tv Online ilifika eneo la tukio na kushuhudia jinsi nyumba hizo zilivyokuwa zikibomolewa, huku wananchi wengi waliokumbwa na patashika hiyo, wakiililia serikali yao, kwani hawakupewa hata muda wa kuhamisha chochote kutoka kwenye nyumba zao.

Jeshi la polisi lilikuwepo eneo la tukio ambapo askari waliojihami kwa bunduki na mabomu ya kutoa machozi, walikuwa wakirandaranda huku na kule, kuhakikisha hakuna anayejitokeza kupinga zoezi hilo.
Tazama video kuona jinsi bomoabomoa hiyo ilivyokuwa.





