×

Makamu wa Rais, Spika Mstaafu Waomboleza Msiba wa George Kahama

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha maombolezo ya Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa kwanza katika serikali ya awamu ya kwanza, Sir George Kahama ,nyumbani kwa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akimfariji mjane wa Marehemu Sir George Kahama Bibi.Janet Bina nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Spika Mstaafu, Anne Makinda akisaini katika kitabu cha maombolezo cha Sir George Kahama nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam leo.

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, Samia Suluhu na Spika Mstaafu wa Bunge la Awamu ya Nne, Anne Makinda, wamefika nyumbani kwa Marehemu George Kahama kwa ajili ya kutoa pole kwa wafiwa.

Spika Mstaafu, Anne Makinda akimfariji mjane wa marehemu Janeth Kahama.

Marehemu George Kahama  enzi za uhai wake alikuwa Waziri na Mwanasiasa Mkongwe. Aidha mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Mke wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Regina Lowassa (wa pili kulia), akiwa kwenye msiba huo

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana mwili  wa marehemu utawasili nyumbani kwake eneo la Mikocheni B kituo cha mabasi kijulikanacho kama Business leo hii saa 11 jioni na kukesha hadi asubuhi.

Sophia Simba akisalimiana na aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Bakari Mwapachu katika msiba huo.

Kesho mwili wa marehemu  utaondolewa nyumbani kwake kuelekea Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) kuanzia  saa mbili kamili kwa ajili ya viongozi mbalimbali na wananchi kutoa heshima zao za mwisho kabla ya kuelekea Kanisa la Mtakatifu Petro ( St. Peters) Oysterbay Dar es salaam saa tano nanusu 5.30 asubuhi kwa ibada.

Baadhi ya Waombolezaji wakiwa msibani

Ibada ya mazishi  itafanyika  katika  makaburi  ya Kinondoni kuanzia saa tisa na nusu  9.30 alasiri.

Marehemu Sir George Kahama enzi za uhai wake.