The House of Favourite Newspapers

Cristiano Ronaldo Anazidi Kuwanyoosha Tu, Kanyakua Tuzo 11 Katika Kipindi cha 2016/2017

MKALI wa kufumania nyavu kutoka Kikosi cha Taifa cha Ureno anayeikipiga kunako Klabu ya Real Madrid inayoshiriki Ligi Kuu ya Hispania, LaLiga, Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Ureno huku akiwaburuza akina Pepe.

Mkali mwingine Renato Sanchez ameshinda tuzo ya mchezaji bora mwenye umri chini ya miaka 21.

Fernando Santos

Mkali huyo anayeingiza mkwanja zaidi kwa wacheza soka Barani Ulaya, ametangazwa mshindi wa tuzo hiyo wakati kocha wa timu ya taifa ya Ureno aliyowaongoza kushinda Kombe la Euro 2016, Fernando Santos akishinda tuzo ya kocha bora wa mwaka. Hii ni tuzo ya 11 ya Ronaldo toka 2016/2017 baada ya tuzo ya mchezaji bora wa Dunia wa FIFA aliyoichukua January 9 2017

Tuzo ya mwanasoka bora wa dunia wa Globe Soccer Award kwa mwaka 2016 inakuwa ni tuzo ya 9 kwa Ronaldo kwa mwaka 2016, baada ya kushinda tuzo za mchezaji bora wa Ulaya, The World SoccerFour Four TwoEspyDi Stéfano AwardGoal.com awardFIFA Club Golden Ball na Ballon d’Or.

 

Comments are closed.