×

Breaking News: Hatimaye Mbunge Peter Lijuakali Kuachiwa Huru

DAR ES SALAAM: Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali (CHADEMA) anatarajiwa kuachiwa huru baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutengua hukumu ya kifungo cha miezi sita aliyohukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Kilombero mwezi Januari mwaka huu.

Peter Lijualikali (30) na Dereva wake, John Kibasa walihukumiwa kwenda jela miezi sita bila faini kwa kosa la kufanya vurugu na kusababisha taharuki katika maeneo ya Ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Kilombero wakati wa kipindi cha uchaguzi mwaka 2015.

Hukumu hiyo ilitolewa Januari 11, 2017 katika Mahakama ya Wilaya ya Kilombero na sasa amepelekwa gerezani ambapo hukumu hiyo ilisomwa chemba lakini wabunge wawili wa Chadema, Joseph Haule (Mikumi) na Ester Bulaya (Bunda Mjini) waliingia na kusikiliza hukumu.

Imeandikwa na Edwin Lindege

Habari hii kusoma kwa undani zaidi cheki Facebook page ya @Gazeti la Ijumaa Wikenda

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaa, muziki na nyingine kali zikufikie kwa wakati.