
Na HAMIDA HASSAN| IJUMAA WIKIENDA| TOWN STORY
DAR ES SALAAM: kufuatia stress (msongo?) za maisha Bongo, Super woman wa sineza za Kibongo, Wastara Juma amekimbilia nchini Sweden kwa madai ya kwenda kuonja maisha ya huko baada ya kupitia mambo mengi mabaya ya kimapenzi na kimaisha.

Akizungumza na Wikienda mubashara kutoka nchini Sweden, Wastara alisema kuwa amegundua akiwa nje ya nchi anapumzika na mengi hasa stress za maisha hivyo kwa mwaka huu ndiyo nitolee kwani hatarajii kurudi tena Bongo hadi mwakani. Alisema katika ziara yakeUlaya anatarajia kusafi ri nchi tatu tofauti.
“Unajua maisha ya Bongo kwa sasa yamejaa vurugu, ni magumu na ukichanganya na stress za mapenzi, nimeona bora nijikalie huku, nafaidi chakula cha mke wa Cloud 112 (Cloud ndiye mwenyeji wake) na kazi zangu za fi lamu zinakwenda kama kawaida tena kwa levo ya juu,” alisema Wastara.
Alipoulizwa hatima ya mpenzi wake, Bond alisema kuwa amempa majukumu ya kuangalia familia na kusimamia miradi yao ya mashamba na production, vitu ambavyo anaamini vitamfanya awe bize muda wote.