×

Video: Duka la Kisasa la GSM Mall Lashika Moto Dar

 Magari ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yakiwa nje ya duka kubwa la GSM Mall, tayari kuzima moto uliokuwa unaunguza duka hilo katika Barabara ya Nyerere eneo la Mtava, Dar es Salaam. Chanzo cha moto huo hakikuweza kujulikana mara moja.

 Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo akiwahishwa hospitali.

 Pilikapilika katika lango kuu la kuingilia duka hilo.

 Mmoja wa majeruhi akitolewa kwenda kwenye gari ili awahishwe hospitali kwa matibabu.

Wananchi wakishuhudia ajali hiyo ya moto

Na Richard Mwaikenda
DUKA kubwa la GSM Mall lililopo Barabara ya Nyerere, eneo la Mtava, Dar es Salaam, limeungua kwa moto leo mchana.

Kwa mujibu wa mashuhuda, duka hilo lilianza kuungua majira ya 8;30 mchana ambapo bado chanzo cha moto huo hakijajulikana.

Wafanyakazi wa duka hilo walionekana kutoka mbio kuokoa maisha yao. Baadhi yao walitolewa wakiwa mahututi na kukimbizwa hospitali kwa kutumia magari ya polisi.

Duka hilo kubwa la kisasa lenye maduka yenye aina mbalimbali za bidhaa ni moja kati ya maduka makubwa yaliyopo jijini Dar es Salaam.

Waokoaji waliokuwepo wamepata wakati mgumu kuzima moto kutokana na ndani ya jengo hilo kuwa na giza nene lililotawaliwa na wingu la moshi uliosababishwa na moto huo.

Wamejitahidi kupata mwanga kwa kuwasha taa za magari karibu na lango kuu la kuingilia ndani lakini ilishindikana.

Leave a Comment