×

MCT Watangaza Wanaowania Tuzo za Umahiri Uandishi wa Habari


Baraza la Habari Tanzania (MCT)  wametangaza majina ya wateule wanaowania Tuzo za Umahiri katika tasnia ya uandishi wa habari.

Akizungumza jijini Dar es Salaam  jana Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi wa Tuzo hizo, Kajubi Mukajanga amesema  kuwa wateule  wanawania tuzo hizo katika madaraja 19  ambapo majaji wamepitia kazi zinazowania kuanzia April 6 hadi 13 mwaka 2017.

Amesema kuwa jumla ya wateule 66 kati yao 36 kutoka magazeti 36, Radio 16 ambapo kati ya wateule 20 ni wanawake na tisa kati yao ni wa magazeti na kumi na moja ni wa vyombo vya eletroniki.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi wa Tuzo hizo, Kajubi Mukajanga akizungumza na wanahabari.

Kajubi amebainisha kuwa idadi hiyo inaonyesha kushuka kwa wateule kulinganisha na Ejat iliyopita ambapo kulikuwa na wateule 84 na kwamba kwa mujibu wa majaji wamesema  kazi nyingi zilizowasilishwa na elektroniki  hazikuwa na ubora ukilinganisha na za magazeti.

Amesema  jumla ya kazi 810 ziliwasilishwa EJAT  mwaka 2016 ikiwa ni ongezeko la kazi 232 kulinganisha na kazi 568 zilizowasilishwa mwaka 2015 na kusema kuwa kati ya kazi 810 kazi 374 ni za magazeti na runinga na radio 435 hali hiyo ikiwa ni mwelekeo mzuri kwa waandaaji Baraza la habari Tanzania.

Aidha amesema shughuli rasmi ya kuwatambua wateule hao zitafanyika rasmi Jumamosi.

VIDEO: MCT Watangaza majina ya wateule Tuzo za uandishi wa habari

Leave a Comment