The House of Favourite Newspapers

Kabula Amchana Live Mr. Chuz

0
Msanii wa kitambo kwenye anga la sinema Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’.

SANII wa kitambo kwenye anga la sinema Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ amemchana live mzazi mwenzie ambaye pia ni msanii mwenzake, Jumanne Kihangala ‘Mr. Chuz’ kwa kumtaka aoe, aache kutangatanga.
Kabula alimpa makavu hayo baba mtoto wake huyo baada ya Chuz kumtumia ujumbe wa kuwa amempata mwanamke ambaye anafanana na yeye hivyo atampelekea amuone ili kama anafaa afunge naye ndoa.

Jumanne Kihangala ‘Mr. Chuz’.

“Unajua Chuz mimi nashangaa umri unaenda sana sasa hivi anatakiwa aoe awe na mke maana kuna kipindi kinafi ka mtu unakua na unaacha kila kitu cha dunia nyuma kwanza halafu unaendelea, sasa Chuz sijui kwa nini hataki kubadilika?” alihoji Kabula. Hata hivyo, alipotafutwa Mr. Chuz hakutaka kuzungumzia suala hilo.

Leave A Reply