Leo ni maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani, ambapo Tanzania inaunga na nchi nyingine duniani kuadhimisha na Kitaifa maadhimisho hayo yanafanyika katika viwanja vya Ushirika Moshi, mkoani Kilimanjaro na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ndiye mgeni rasmi katika maadhimisho hayo akiwa ameambatana na Makamu wa Rais, Samia Suluhu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Spika Job Ndugai, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecky Sadick pamoja na viongozi wengine wa Kitaifa.
Akizungumza wakati akiwahutubia wananchi kwenye hafla hiyo, Rais Magufuli ameyasema haya
“Kuna wafanyakazi wengine wamezeeka kabisa na muda wao wa kustaafu umeshapita lakini wamebadilisha umri wao ili waendelee kufanya kazi, hao nao ni hewa ni tutawashughulikia hivi karibuni.
“Hapa kwetu Tanzania, hakuna sheria inayosema kwamba kuajiriwa lazima uwe na digri, kila mmoja aombe kazi inayoendana na elimu yake, kama wewe elimu yako ni darasa la saba uombe kazi inayoendana na darasa la saba, kama ni digrii au diploma hivyo hivyo.
“Wenye vyeti vya kugushi watupishe.
“Nataka kuwahakikishia wafanyakazi tunaanza ukurasa mpya, utatu ujengwe kikamilifu kati ya mfanyakazi, mwajiri na serikali.
“Naagiza mwanamke aliyebeba bango la kuomba asaidiwe juu ya mirathi ya mumewe, suala lake lishughulikiwe.

“Hivi karibuni baada ya kuzindua ubalozi Israel, tumepokea watalii 800 na kutoka nchini humo, na wengine 300 wanakuja.
“Vyama vya wafanyakazi visigeuzwe kuwa sehemu ya migogoro na migomo.
“Sikutaka kupandisha mishahara kwa sababu nilipanga nisafishe kwanza nisiongezea mishahara watu wasiostahili kupata.
“Nitatoa ongezeko la kawaida la mshahara kila mwaka Annual increment na promotions zote zilizokuwa zimesiama.

“Serikali itahakikisha kuwa, hakuna mfanyakazi atakayehamishwa kuanzia sasa bila kupewa fedha zake za uhamisho.
“Serikali inaandaa muswada wa uanzishwaji wa bima ya ajira mara utakapokamilika utawasilishwa bungeni kujadiliwa.
“Kuanzia bajeti ijayo, serikali itaongeza mishahara ya wafanyakazi kutoka kiwango kilichokaa kwa muda mrefu.