×

VIDEO: Mwakyembe Apokea Mil.12 Kuisaidia Serengetiti Boys

Mkurugenzi wa Idara ya Maelezo, Abbas Hassan aliyekabidhi hundi kwa niaba ya Multi choice.


DAR ES SALAAM: Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amepokea msaada wa shilingi Million 12 kutoka kwa wadau watatu kwa ajili ya kuisaidia Timu ya Taifa ya Vijana Chini ya Miaka 17 ‘Serengeti Boys’.

Akizungumza wakati wa kupokea misaada hiyo, Mwakyembe alilsema bado kunahitajika jitihada za pamoja kutoka kwa wadau mbalimbali katika kuiunga mkono timu hiyo ili iweze kufanya vizuri katika Michuano ya Kimataifa inayoendelea nchini Gabon.

Salome Kitomari kutoka Misa Tan.

Waliyoichangia Serengeti Boys ni Kampuni ya Multichoice Tanzania iliyochangia Tsh. Mil. 10, Taasisi ya Vyombo vya Vabari Kusini mwa Afrika (Misa Tan) waliochangia Tsh. Mil. 1, na Mkurugenzi wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU aliyechangia Tsh. Mil. 1.

Katika mechi yake ya kwanza iliyopigwa jana, Serengeti Boys walitoka sare ya bila kufungana na Bingwa Mtetezi wa mashindano hayo, Mali.

NA DENIS MTIMA | GPL

Leave a Comment