




Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita Charles jana amekabidhi rasmi magari mawili aina ya Suzuki Carry maarufu kama (Kirikuu) kwa washindi wa shindano la shika ndinga linaloandaliwa na kuendeshwa na kituo cha utangazaji cha EFM redio, washindi waliopatikana katika fainali iliyofanyika tarehe sita mwezi wa tano mwaka huu katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe Jijini Dar es Salaam.