×

Mazishi ya Aliyechora Nembo ya Taifa, Misungwi, Mwanza leo

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella akitoa salamu za rambirambi kwa niasa ya serikali ya mkoa na Rais John Magufuli wakati wa mazishi ya mbunifu wa Nembo ya Taifa, Francis Maige ‘Ngosha’ leo huko Misungwi, Mwanza.
Familia ya marehemu Francis Maige ‘Ngosha’ na baadhi ya waombolezaji.

Mwakilishi wa Wizara ya Afya Jinsia na watoto Beatrice Singano akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Francis  Maige ‘Ngosha’akifuatiwa an Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Clowdwing Mtweve janaa.
Baadhi ya waombolezajiwakiwa wamebeba jeneza na mwili wa marehemu Francis Maige ‘Ngosha’ kuelekea kwenye makaburi ya familia.
Casmir Masolwa ambaye ni mpwa wa marehemu Francis Maige ‘Ngosha’ akiweka mchanga kwenye kaburib wakati wa mazishi ya mjomba wake yaliyofanyika kwenye makaburi ya familia katka kijiji cha Igokelo.
Maombi ya yakiendelea kabla ya maziko.
Baadhi ya waombolezaji kishusha kaburini jeneza la mwili wa marehemu.
Mbunge wa Misungwi, Charles Kitwanga kushoto, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella katikati, na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Sweda kulia wakiweka shada la maua kwenye kaburi la Francis Maige leo wakati wa mazishi yake.

 

Dada wa marehemu Maige, Maria Ihenyale kushoto na mwanaye Casmir Masolwa wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mbunifu huyo wa Nembo ya Taifa.​

 Marehemu Mzee Francis Maige Kanyasu almaarufu Ngosha, aliyekuwa akidai kwamba ni miongoni mwa watu waliobuni na kuchora nembo ya taifa, aliyefariki dunia usiku wa Mei 29, 2017 kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa akitibiwa amezikwa leo kijijini kwao Misungwi, Mwanza.

(PICHA NA IDD MUMBA NA MASHAKA BALTAZAR, MWANZA)

Leave a Comment