The House of Favourite Newspapers

Breaking News: CUF ya Prof. Lipumba Yamaliza Mgogoro na CUF ya Maalim Seif

1

CUF – CHAMA cha Wananchi, upande unaoungwa mkono na Profesa Ibrahim Lipumba, kimetangaza kumaliza mgogoro uliokuwa ukifukuta ndani ya chama hicho na kwamba tayari wameshaunda bodi halali iliyosajiliwa na RITA.

 

Abdul Kambaya, Mwenyekiti wa Habari na Uenezi wa CUF ambaye ndiye aliyekuwa mzungumzaji mkuu kwenye mkutano na waandishi  amesema kuwa, bodi hiyo itadumu kwa miaka mitano hivyo kuwataka upande wa pili wanaomuunga, mkono Katibu Mkuu, Maalim Seif wakutane na upande wa Lipumba wake meza moja kwa ajili ya majadiliano pamoja na kukijenga chama hicho upya.

Aidha viongozi hao wameeleza kufurahishwa kwao na vitendo vya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kusimamia rasilimali za taifa yakiwemo madini na kuwataka Watanzania wote bila kujali itikadi ya vyama vyao wamuunge mkono rais.

Pia wamempongeza rais kwa kuwashughulikia ipasavyo mafisadi papa kwa kuwafikisha mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

Ikumbukwe kuwa pande mbili kwa maana ya Wanachama wa CUF wanaomuunga mkono Prof. Lipumba na wale wanaomuunga mkono Maalim Seif wamekuwa katika vuguvugu la kutokuelewana kwa miezi kadhaa sasa tangu Lipumba alivyorudi ndani ya chama na kurudi kwenye kiti chake cha uenyekiti wa chama Taifa.

TAZAMA VIDEO HAPA

1 Comment
  1. […] Furaha na Furaha. Mgogoro huu unasababishwa na Furaha kuanza mienendo mibaya. Suluhisho la mgogoro huu ni Furaha kumkanya […]

Leave A Reply