
MCHUNGAJI Dkt. Huruma na Mchungaji Joyce Nkone wa Victory Christian Centre (VCC) Tabernage wametayarisha tamasha la Mwezi wa Familia la wiki nzima tangu Julai Mosi na kumalizika Julai 30 mwaka huu.
Tamasha hilo litafanyika Mbezi Beach A, Barabara ya Mwai Kibaki, Mtaa wa Kilimani Close baada ya daraja la Mto Mbezi jijini Dar es Salaam.
Tamasha hilo ambalo litafanyika kuanzia siku za Julai Mosi, 8, 15 na 22 na ambalo linawaalika watu wote, litajumuisha mafunzo ya Shule ya Ndoa kwa Wanandoa (Marriage School) ambayo itafanyika tangu saa 02:30 hadi 04:00 asubuhi
Kutakuwepo pia Maombi na Maombezi kwa Familia na Ndoa kuanzia saa 4:30 asubuhi hadi saa 6:30 mchana katika tarehe zote hizo.
Ratiba ya tamasha hilo inasema kuwa kuna Karamu ya Wanandoa (Couples Banquet) itakayofanyika Ijumaa Julai 28 kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 5:00 usiku.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa, siku ya Jumapili Julai 30, kutakuwa na Ibada ya Familia (VCC Family Service) itakyoanzasaa 2:00 asubuhi hadi saa 7:00 mchana.
Kwa kupata habari zaidi kuhusu tamasha hilo watakaohudhuria wapige simu kupigia namba 0714 503638 na 0762 441719, baruapepe [email protected] au kufika Victory Christian Centre (VCC).