
JEURI YA PESA! KLABU ya Singida United ambayo imepanda daraja msimu uliopita, ikiwa kwenye maandalizi ya michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara, leo imezidi kuonyesha jeuri yake ya pesa baada ya kuwashusha rasmi wachezaji wake wapya wawili kutoka nchini Rwanda.

Michael Rusheshangonga ambaye ni beki kisiki wa kulia wa timu ya Taifa ya Rwanda na nahodha wa APR ya nchini humo amekabidhiwa jezi yake namba 22 mara tu baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar.

Rusheshangonga ambaye ametwaa tuzo ya Goli bora la msimu kwa ligi kuu ya Rwanda atua nchini na kwenda moja kwa moja kuungana na wenzake walipo kambini Mwanza.

Kwa hatua nyingine, yule mfungaji bora wa Ligi Kuu Rwanda kwa misimu miwili mfululizo, Dany Usengima naye ametua Singidani leo.
Usengimana ametua nchini leo mchana na moja kwa moja kutambulishwa kwa kukabidhiwa jezi namba 10 ya Singida United.
Singida United wanaodhaminiwa na SportPesa, wameamua kuingia kwa fujo kwenye Ligi Kuu Bara baada ya kupanda tena msimu ujao.

Wanyarwanda hao wanatarajia kutoa ushindani mkubwa katika “kuchana” nyavu kwa msimu ujao na leo wameungana rasmi na kikosi hicho.
Dany Usengimana, Mchezaji huyo ambaye ni tegemeo kwa timu ya Taifa ya Rwanda ameingia mkataba wa kuitumikia Singida United kwa miaka miwili kwa dau nono.
Singida united iliyopo Mwanza, inaelekea kwishi kabisa katika usajili wake wa kuimarisha kikosi tayari kwa mapambano ya Ligikuu msimu wa 2017/2018 Tanzania bara.
PICHA ZOTE NA MUSA MATEJA | GLOBAL PUBLISHERS