
Mshambuliaji hatari aliyekuwa Manchester United na kuhamia Everton wiki iliyopita Wayne Rooney, ametua Bongo akiwa na klabu yake mpya ambayo inatarajiwa kukipiga na Gor Mahia katika mechi ya mdhamini wao, Sport Pesa kwenye dimba la taifa jijini Dar es Salaam.
Rooney, wachezaji wenzake wa Everton na benchi la ufundi, waliwasili asubuhi ya leo ambapo baada ya mapumziko mafupi, jioni walirudi uwanjani hapo kwa ajili ya mazoezi mepesi.
Hiki hapa kikosi kamili cha Everton waliowasili Tanzania leo:
Maarten Stekelenburg, Mateusz Hewelt, Chris Renshaw, Tom Davies, Phil Jagielka, Ashley Williams, Callum Connolly, Jonjoe Kenny, Michael Keane, Muhamed Besic, Leighton Baines, Morgan Schneiderlin, James McCarthy, Davy Klaassen, Gareth Barry, Idrissa Gana Gueye, Joe Williams, Kieran Dowell, Kevin Mirallas, Wayne Rooney, Aaron Lennon, Dominic Calvert-Lewin, Ademola Lookman, Matthew Pennington, Yannick Bolasie.