






Familia ya Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Harisson Mwakyembe, imepatwa na msiba mkubwa baada ya kuondokewa na mpendwa wao, Lina Mwakyembe, ambaye ni mke wa waziri huyo.
Lina amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua kwa muda mrefu saratani ya titi.
Kwa mujibu wa msemaji wa familia, Solomon Kivuyo, marehemu Lina alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa huo kwa muda mrefu karibu miaka miwili akiwa anatibiwa hospitali mbalimbali duniani.
Pia, alishawahi kulazwa katika hospitali za Muhimbili, Aga Khani, India na Uturuki.
Marehemu anatarajiwa kuzikwa Kyela, mkoani Mbeya, siku ya Jumatano ijayo .
Na Issa Mnally | Global Publishers | Dar es Salaam