LIVE NGUMI ZA GLOBAL TV: NASIBU RAMADHANI VS YOHANE BANDA
TAZAMA LIVE MARUDIO YA MPAMBANO WA NASIBU RAMADHANI VS YOHANE BANDA KUPITIA GLOBAL TV ONLINE
JUMLA ya mabondia sita usiku wa kuamkia jana walipanda ulingoni katika mapambano ya kimataifa ya ubingwa wa Global TV, Afrika Mashariki na Kati kwenye Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijjini Dar na kufanya mambo makubwa.
Ndonga hizo zilikuwa na mvuto wa kipekee, zilishuhudia mabondia Watanzania wawiki wakishinda na mmoja kupata sare ulingoni mbele mashabiki waliojitokeza ukumbini hapo huku wengine wakifuatilia kupitia chaneli ya YouTube ya Global TV Online.
NASIBU RAMADHANI VS YOHANE BANDA
Mtanzania Nasibu Ramadhani alifanikiwa kushinda kwa TKO katika raundi tisa baada ya mpambano kuwa kali. Mabondia hao walionyeshana umwamba kuanzia raundi ya kwanza lakini alikuwa ni Nasibu ndiye aliyeonekana kuwa fiti zaidi kutokana na kuonyesha kujiamini muda mwingi wa mchezo.
Banda ambaye ni Mmalawi alianguka mara kadhaa na ilipofika raundi ya 9 makonde yakazidi na kuanguka zaidi ya mara mbili ndipo mwamuzi akaingilia na kumuokoa.