Kufuatia skata la kesi ya Wema Sepetu ambaye anadaiwa mkojo wake ulikutwa na chembechembe za bangi baada ya kupimwa na Mkemia Mkuu, Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amefafanua juu ya vipimo vinavyohusiana na mkojo hasa katika watuhumiwa mbalimbali wanaofikishwa mahakamani kwa matumizi ya dawa za kulevya.