×

‘Wabunge’ Waropokaji, Wanaosinzia Wakiona cha Mtema Kuni

Bakora Comedy Show, ni kipindi chenye kuelimisha na kufikisha ujumbe kwa wananchi kwa njia ya vichekesho ambapo leo, waheshimiwa wabunge walikuwa wakichangia mada bungeni kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu elimu lakini miongoni mwao, walikuwepo waliokuwa wakileta masihara bungeni.

 

Wengine walikuwa wakichangia hoja katika namna ya kushangaza kabisa, wakitetea mambo ambayo ni kinyume na maadili ya Kitanzania, wengine wakafikia hatua ya kurushiana viatu na makaratasi bungeni, huku wengine wakipiga kelele hovyo.

 

Mwisho wa yote, mwakilishi wa wananchi, akaingia akiwa na azimio la alichotumwa na wananchi ambapo, alianza kwa kueleza jinsi ambavyo wabunge hao walipaswa kuwasilisha hoja walizotumwa na wananchi, mwisho akaamua kuwawashia moto wote waliokuwa wakileta masihara bungeni, kwa kuwacharaza fimbo bungeni, tena wakiwa wanaoneshwa moja kwa moja na runinga.

Ni shoo ya kuchekesha itakayokuwa ikikujia kupitia Global Tv Online.

 

Bakora Show;’Wabunge’ Waropokaji, Wanaosinzia Wakiona cha Mtema Kuni, Wacharazwa Fimbo Bungeni

Leave a Comment