
Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) ilitarajia kupokea fomu zote za matokeo kutoka vituo vya kupigia kura kufikia leo saa sita mchana. Tangazo la mshindi wa urais linatarajiwa kutolewa baada ya tume hiyo kuhakiki fomu hizo.
Ofisa Mkuu Mtendaji wa IEBC, Ezra Chiloba, amesema tume hiyo sasa imefanikiwa kupata fomu za matokeo kutoka majimbo 288 ya uchaguzi.
Amesema Fomu 34B za maeneo mawili bado haziko tayari. Hata hivyo amesema wameziona fomu hizo na wamewasiliana na wasimamizi wa uchaguzi maeneo hayo mawili. Hata hivyo, kulikuwa na mambo yaliyohitaji kufafanuliwa kwenye fomu hizo.
Chiloba amewaomba Wakenya kuwa na subira akaongeza kwamba: “Ni muhimu zaidi tuwe sahihi kuliko kuharakisha.”
Matokeo yatatangazwa muda wowote kuanzia sasa.