×

Rais Abdel Fattah Al Sisi wa Misri Kuzuru Tanzania Wiki Ijayo

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Aziz Mlima akizungumza na wanahabari.

RAIS wa Misri, Abdel Fattah Al Sisi anatarajiwa kufanya ziara nchini hapa kuanzia wiki ijayo. Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Aziz Mlima, amesema ziara hiyo itakuwa ni ya kwanza nchini tangu Rais John Magufuli aingie madarakani.

Dkt. Aziz Mlima akizungumza na wanahabari.

Alisema lengo la ziara hiyo ni kuimarisha na kukuza uhusiano wa kidiplomasia, kiuchumi na kijamii kati ya nchi hizi mbili. Ziara hiyo pia itatoa fursa kwa viongozi kujadili masuala mbalimbali ya kikanda na kimataifa yanayohusu nchi hizo mbili.

Leave a Comment